The Most Embarrassing Moment of My Life – Devil Artworks

The Most Embarrassing Moment of My Life
The Most Embarrassing Moment of My Life

The Most Embarrassing Moment of My Life… Yaani nime realize hii life usipo kaa rada shetani anaeza design siku yako from morning hadi jioni. Nakumbuka nikiamka nilikuwa na kauvivu kiasi, roho inaniambia nisiende job, ingine inaniambia niende coz I bought a new wig at least I showoff (Diganithie).

Mimi huyoo mbio mbio kujitayarisha, chai singekunywa ya home coz nilitaka kufika mapema kila mtu anione. Kiatu nikatafuta high heel coz lazima ningemeet all specification za kuitwa slay queen.

But why did I forget to say a word of prayer? …mimi huyo mpaka kwa gari, all eyes were on me and u know ka feeling, I felt like introducing myself as (Mwari wa Kenyatta)… The guys who were staring at me, I felt like asking them (Mwina besha kana no wanna)? But fyuux…

Nakumbuka am a mother’s Union member… Nikachukua simu yangu kuanza kuchat na mabesty, little did I know nishapeanwa kama dhabihu mikononi mwa adui… Kijamaa kinaingia kwa mat akiongea na simu, kidogo kidogo jamaa akiwa kwa process ya kutafuta kiti dere akaona makarao akawasha gari faster…

Jamaa alinishika kichwa akaanguka chini na wig yangu… hata shida si kuanguka ndani ya gari, ata shida si kuumia kwake, shida ni wig yangu iliingia chini ya viti na hakujua haswa imeanguka wapi… aliamka na aibu za kuanguka na badala ya anyamaze, akaambia abiria wote kila mtu aangalie chini kama kuna nywele ataona anipee…

“Madam am soo sorry, but mbona hujachana nywele?” How did he expect me to answer that kind of a question?… how embarrassing…. wig yangu ilitafutwa na kila mtu hadi makanga… kwa bahati acha niseme ni (bahati mbaya) ikapatikana, kila mtu kwa gari alikuwa amemtazama kwa mshtuko, jamaa badala akae nayo atleast anipatie ki mpango, alikuja akanipee na akaniambia… “pole sana madam sikukusudia kufanya hivyo, but usivae imekanyangwa na matope… niruhusu nikulipie fare” nikachukua mzigo wangu nikaeka kwa bag.

Kwa kichwa nikasema hata mbuzi huwa inatembea na nywele haijachanwa… kila mtu alinicheka kwa hio gari including wale majamaa walikuwa wananicheki likely to suggest wanataka number yangu ya simu…sasa sijui kama ni mimi walichekelea ama ni mwenye alianguka…

Nilichukua earphones nikaeka kwa maskio nikafunga macho na nikaanza kuskiza (Dance ya Kanisa) niliamshwa na mwenye tulikuwa tumekaa karibu naye akaniambia ”tumefika town Madam ama umepitishwa”?

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*